DJM/2024/0235 BENEDICT BANABA MNALI
KIJANA ANAEJISHUGHULISHA NA SANAA YA MITINDO YA NYWELE
Kijana anaetambulika kwa jina la Johnson Kimaro mwenye umri wa miaka 28 ambae ameamua kujishughulisha na sanaa ya mitindo ya nywele yaani ususi anaepatikana maeneo ya Nganza ambapo kazi yake hiyo inamuingizia kipato katika kazi yake Pamoja na kuendesha familia yake licha ya kuwa anapitia changamoto mbalimbali kwenye kazi hiyo
CHANGAMOTO ANAZOZIPITIA JOHNSON KIMARO
Licha ya ufanisi mkubwa anaoufanya Johnson katika kazi yake,pia kuna baadhi ya changamoto mbalimbali anazozipitia,ikiwemo ya kudharaulika katika jamii kwani watu wengi wanaamini kazi hiyo ni mahususi kwa wanawake tu kwani imezoeleka hivyo,pia mbali na hiyo jambo lingine ambalo linamletea shida ni kwa upande wa wasichana ambao hufanya nao kazi na kutaka kumpatia rushwa ya ngono(kimapenzi).



Comments
Post a Comment