Posts

Showing posts from November, 2024

DJM/2024/0127 ANETH FABIANI KALINGA

Image
          ULEMAVU SI UGONJWA Kuna wimbi kubwa la watu nchini wenye Imani potofu juu ya watu wenye ulemavu,wakiamini kuwa watu wenye ulemavu hawastahili kupewa haki sawa na watu wasio na ulemavu,ambapo Imani hiyo imekuwa si ya kweli,kwani watu wenye ulemavu wana haki sawa na watu wengine wa kawaida,pengine watu wenye ulemavu wanastahili kupewa kipaumbele zaidi katika nyenzo mbalimbali. Na leo hii kutana na kijana Francisco kimila mkazi wa nyamalango mwenye umri wa miaka 25 ni mwanafunzi wa chuo cha mtakatifu Agustine mwenye changamoto ya ulemavu wa mkono pamoja na mguu,ambapo anatueleza mambo mbalimbali katika safari yake ya maisha hadi sasa,licha ya changamoto zote anazozipitia lakini bado hajakata tamaa katika kupambania ndoto zake.                Francisco kimila joachim  CHANGAMOTO ANAZOZIPITIA KIJANA Francisco Katika upande wa changamoto anazozipitia Francisco ni pamoja na suala la ufuaji wa nguo zake,kwani kuto...

DJM/2024/0235 BENEDICT BANABA MNALI

Image
     KIJANA ANAEJISHUGHULISHA NA SANAA YA MITINDO YA NYWELE Kijana anaetambulika kwa jina la Johnson Kimaro mwenye umri wa miaka 28 ambae ameamua kujishughulisha na sanaa ya mitindo ya nywele yaani ususi anaepatikana maeneo ya Nganza ambapo kazi yake hiyo inamuingizia kipato katika kazi yake Pamoja na kuendesha familia yake licha ya kuwa anapitia changamoto mbalimbali kwenye kazi hiyo CHANGAMOTO ANAZOZIPITIA JOHNSON KIMARO Licha ya ufanisi mkubwa anaoufanya Johnson katika kazi yake,pia kuna baadhi ya changamoto mbalimbali anazozipitia,ikiwemo ya kudharaulika katika jamii kwani watu wengi wanaamini kazi hiyo ni mahususi kwa wanawake tu kwani imezoeleka hivyo,pia mbali na hiyo jambo lingine ambalo linamletea shida ni kwa upande wa wasichana ambao hufanya nao kazi na kutaka kumpatia rushwa ya ngono(kimapenzi). MAONI YA JOHNSON KWA VIJANA WENZAKE Aidha kwa upande mwingine Johnson aliwahasa vijana wenzake kwa kuamini wanachokifanya na kupambania ndoto zao ili wafikishe malengo...